Swali: Ni vipi hutolewa zakaah ya mishahara ya kila mwezi na misaada inayotolewa kwenye mataasisi?
Jibu: Njia bora, nyepesi na ilio salama zaidi ni kutenga mwezi fulani na kutoa zakaah yako yote. Kwa mfano mtu amezowea kila inapoingia Ramadhaan basi anahesabu ile mali alionayo na akatoa zakaah ya mwaka huo kukiwemo Sha´baan ya mwaka huo. Hili ni zuri na linamfanya mtu ahisi afueni. Sijapata njia afueni kuliko hii.
Pengine mtu akasema kuwa kumepita baadhi ya siku tu juu ya mshahara wa Sha´baan, basi tunamwambia kuwa zakaah hiyo inakuwa imeharakishwa na imetolewa kabla ya wakati. Isitoshe inafaa kwa mtu akatoa zakaah yake mwaka mmoja au miwili kabla. Kwa hivyo njia bora ni mtu atenge mwezi fulani awe akitoa zakaah ya mali yake yote na hivyo akaitolea zakaah yake ile pesa ambayo ameihifadhi mwaka mzima na ambayo bado imekamilisha mwaka mzima na ambayo haijakamilisha.
Kuhusu misaada ya mataasisi ambayo huhifadhi pesa kwa ajili ya kusaidia, hawaitolei zakaah.
- Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/175-176)
- Imechapishwa: 07/05/2021
Swali: Ni vipi hutolewa zakaah ya mishahara ya kila mwezi na misaada inayotolewa kwenye mataasisi?
Jibu: Njia bora, nyepesi na ilio salama zaidi ni kutenga mwezi fulani na kutoa zakaah yako yote. Kwa mfano mtu amezowea kila inapoingia Ramadhaan basi anahesabu ile mali alionayo na akatoa zakaah ya mwaka huo kukiwemo Sha´baan ya mwaka huo. Hili ni zuri na linamfanya mtu ahisi afueni. Sijapata njia afueni kuliko hii.
Pengine mtu akasema kuwa kumepita baadhi ya siku tu juu ya mshahara wa Sha´baan, basi tunamwambia kuwa zakaah hiyo inakuwa imeharakishwa na imetolewa kabla ya wakati. Isitoshe inafaa kwa mtu akatoa zakaah yake mwaka mmoja au miwili kabla. Kwa hivyo njia bora ni mtu atenge mwezi fulani awe akitoa zakaah ya mali yake yote na hivyo akaitolea zakaah yake ile pesa ambayo ameihifadhi mwaka mzima na ambayo bado imekamilisha mwaka mzima na ambayo haijakamilisha.
Kuhusu misaada ya mataasisi ambayo huhifadhi pesa kwa ajili ya kusaidia, hawaitolei zakaah.
Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/175-176)
Imechapishwa: 07/05/2021
https://firqatunnajia.com/zakaah-juu-ya-mishahara-ya-mwezi-na-misaada-ya-mataasisi/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)