Swali: Kuna mtu hutoa zakaah kwa ajili ya mshahara wake. Ametenga mwezi maalum wa kufanya hivo kama vile Ramadhaan. Pasi na kujali ana kitu kikubwa au kidogo inapofika Ramadhaan basi hukitolea zakaah. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Ni vizuri na hakuna neno mtu akatenga mwezi fulani kwa ajili ya kutoa zakaah yake. Unapofika mwezi huo basi anakusanya ile mali alionayo na kuitolea zakaah. Anaweza pia kuitolea zakaah ile pesa ambayo haijafikisha mwaka. Uharakishaji huu haudhuru kitu. Uharakishaji huu aliotaja unawanufaisha mafukara.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/179-180)
  • Imechapishwa: 07/05/2021