Zakaah inagawanywa kupitia jumuiya ya zakaah

Swali: Wakati kiwango cha pesa kinapotimiza mwaka, mtoa zakaah anaitoa kuwapa jumuiya ya zakaah. Je, ni wajibu kwa jumuya hiyo kuitoa papo hapo au jambo hilo ni lenye wasaa kwa vile wengi wanatoa zakaah zao katika Ramadhaan. Wenye zakaah zao wanaomba pesa zao zitolewe kabla ya kumalizika kwa Ramadhaan. Je, ni wajibu?

Jibu: Ikiwa mtoa zakaah ataweka sharti hiyo, basi jumuiya ya zakaah itamwambia kuwa wao hawawezi kutekeleza sharti hiyo; ima wamwambie kuwa wataigawanya zakaah yake kutokana na haja au aigawanye mwenyewe. Ni wajibu jambo liwe namna hiyo. Haijuzu kwa jumuiya ya zakaah kutoa zakaah za watu za mwaka mzima ikiwa wenye kutoa zakaah hizo wanafikiria kuwa itagawanywa ndani ya Ramadhaan.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/460-461)