Sampuli ya kwanza ya unafiki ni ule unafiki wa kiimani kama tulivosema. Hii ni dhambi kubwa inayomtoa mwenye nayo katika Uislamu. Dalili yake iko wazi kabisa ndani ya Qur-aan:
وَمِنَ النَّاسِ مَن يَقُولُ آمَنَّا بِاللَّـهِ وَبِالْيَوْمِ الْآخِرِ وَمَا هُم بِمُؤْمِنِينَ ﴿٨﴾ يُخَادِعُونَ اللَّـهَ وَالَّذِينَ آمَنُوا وَمَا يَخْدَعُونَ إِلَّا أَنفُسَهُمْ وَمَا يَشْعُرُونَ ﴿٩﴾ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ فَزَادَهُمُ اللَّـهُ مَرَضًا ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ بِمَا كَانُوا يَكْذِبُونَ ﴿١٠﴾ وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ لَا تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ قَالُوا إِنَّمَا نَحْنُ مُصْلِحُونَ ﴿١١﴾ أَلَا إِنَّهُمْ هُمُ الْمُفْسِدُونَ وَلَـٰكِن لَّا يَشْعُرُونَ ﴿١٢﴾ وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ آمِنُوا كَمَا آمَنَ النَّاسُ قَالُوا أَنُؤْمِنُ كَمَا آمَنَ السُّفَهَاءُ ۗ أَلَا إِنَّهُمْ هُمُ السُّفَهَاءُ وَلَـٰكِن لَّا يَعْلَمُونَ ﴿١٣﴾ وَإِذَا لَقُوا الَّذِينَ آمَنُوا قَالُوا آمَنَّا وَإِذَا خَلَوْا إِلَىٰ شَيَاطِينِهِمْ قَالُوا إِنَّا مَعَكُمْ إِنَّمَا نَحْنُ مُسْتَهْزِئُونَ ﴿١٤﴾ اللَّـهُ يَسْتَهْزِئُ بِهِمْ وَيَمُدُّهُمْ فِي طُغْيَانِهِمْ يَعْمَهُونَ ﴿١٥﴾ أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ اشْتَرَوُا الضَّلَالَةَ بِالْهُدَىٰ فَمَا رَبِحَت تِّجَارَتُهُمْ وَمَا كَانُوا مُهْتَدِينَ ﴿١٦﴾ مَثَلُهُمْ كَمَثَلِ الَّذِي اسْتَوْقَدَ نَارًا فَلَمَّا أَضَاءَتْ مَا حَوْلَهُ ذَهَبَ اللَّـهُ بِنُورِهِمْ وَتَرَكَهُمْ فِي ظُلُمَاتٍ لَّا يُبْصِرُونَ ﴿١٧﴾ صُمٌّ بُكْمٌ عُمْيٌ فَهُمْ لَا يَرْجِعُونَ ﴿١٨﴾ أَوْ كَصَيِّبٍ مِّنَ السَّمَاءِ فِيهِ ظُلُمَاتٌ وَرَعْدٌ وَبَرْقٌ يَجْعَلُونَ أَصَابِعَهُمْ فِي آذَانِهِم مِّنَ الصَّوَاعِقِ حَذَرَ الْمَوْتِ ۚ وَاللَّـهُ مُحِيطٌ بِالْكَافِرِينَ ﴿١٩﴾ يَكَادُ الْبَرْقُ يَخْطَفُ أَبْصَارَهُمْ ۖ كُلَّمَا أَضَاءَ لَهُم مَّشَوْا فِيهِ وَإِذَا أَظْلَمَ عَلَيْهِمْ قَامُوا ۚ وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ لَذَهَبَ بِسَمْعِهِمْ وَأَبْصَارِهِمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٢٠
”Miongoni mwa watu wako wasemao: “Tumemuamini Allaah na siku ya Mwisho” hali ya kuwa si wenye kuamini. Wanatafuta kumhadaa Allaah na wale walioamini, lakini hawahadai isipokuwa nafsi zao wala hawahisi. Ndani ya nyoyo zao mna magonjwa na Allaah akawazidishia maradhi na watapata adhabu iumizayo kwa waliyokuwa wakiyakadhibisha. Wanapoambiwa: “Msifanye maharibifu katika ardhi husema hakika sisi ni watengenezaji”. Zindukeni! Hakika wao ndio waharibifu lakini hawahisi. Wanapoambiwa: ”Aminini kama walivyoamini watu” husema: ”Je, tuamini kama walivyoamini wapumbavu?” Zindukeni! Hakika wao ndio wapumbavu lakini hawajui. Wanapokutana na wale walioamini husema: ”Tumeamini.” Na wanapokuwa peke yao pamoja na mashaytwaan wao, husema: ”Hakika sisi tuko pamoja nanyi, hakika sisi ni wenye kuwadhihaki tu.” Allaah anawadhihaki wao na atawawacha katika upotevu wao wakitangatanga ovyo. Hao ndio walionunua upotofu kwa uongofu, basi haikupata faida biashara yao na wala hawakuwa wenye kuongoka. Mfano wao ni kama mfano wa aliyekoka moto, ulipoyaangaza yaliyopo pembezoni mwake Allaah akawaondoshea nuru yao na akawaacha katika viza na hawaoni. Viziwi, mabubu, vipofu basi hawatorejea. Au ni kama mvua kubwa kutoka mbinguni, ndani yake mna viza na radi na umeme, wanatia vidole vyao katika masikio yao kutokana na mingurumo wakikhofu mauti; Allaah ni Mwenye kuwazunguka makafiri. Unakaribia umeme kunyakua macho yao, kila unapowaangazia njia hutembea humo, na unapowafanyia kiza husimama. Lau Allaah angelitaka, basi angeliwaondoshea kusikia kwao na kuona kwao. Hakika Allaah juu ya kila jambo ni Muweza.”[1]
Aayah hizi zinafichua siri, uwongo, kiburi, uwoga wao na uadui wao mkubwa dhidi ya Uislamu na waislamu, kama zilivyokuja Aayah kadhaa katika Suurah “at-Tawbah” na Suurah kamili kwa jina “al-Munaafiquun”.
[1] 02:08-20
- Muhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 162-163
- Imechapishwa: 24/06/2026

Muhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 162-163
Imechapishwa: 24/06/2026
https://firqatunnajia.com/72-mfano-wa-unafiki-wa-wanafiki/