Ni muhimu kujua kuwa unafiki umegawanyika aina mbili:
1 – Unafiki wa kiitikadi ambao punde tumetoka kuuzungumzia. Aina hii ya unafiki unamtoa mwenye nao katika Uislamu na mwenye nayo ni miongoni mwa viumbe waovu kabisa.
2 – Unafiki wa kimatendo ambao ni miongoni mwa madhambi makubwa, lakini haumtoi mwenye nao katika Uislamu. Aina hii ndio aliyokusudia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pale aliposema:
”Alama za mnafiki ni tatu; anapoongea anasema uongo, anapoahidi anakhalifu na anapoaminiwa anafanya khiyana.”[1]
Imekuja katika tamko jengine:
“… anapogombana, hufanya uovu…”[2]
Imekuja katika tamko jengine:
“… anapoahidi, anasaliti… “
Hapa kumetajwa alama tatu. Huu ndio unafiki wa kimatendo na ni khatari mno, kwa sababu uwongo unapelekea katika maovu. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Jilazimianeni na ukweli. Hakika ukweli unaongoza katika wema na hakika wema unaongoza katika Peo na mtu ataendelea kusema ukweli mpaka aandikiwe mbele ya Allaah kuwa ni mkweli. Hakika uongo unaongoza katika uovu na uovu unaongoza katika Moto. Hakika mtu ataendelea kusema uongo mpaka aandikwe mbele ya Allaah kuwa ni mwongo.”[3]
Uwongo ni miongoni mwa sifa zinazomchafua muislamu, ni mamoja amesema uwongo juu ya Allaah, Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) au kuwasmea uwongo watu. Namna hii ndivo Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanavyogawanya unafiki. Aina zote mbili mafungu yake yamejulishwa waziwazi ndani ya Qur-aan na Sunnah.
[1] al-Bukhaariy (33) na Muslim (59).
[2] al-Bukhaariy (34) na Muslim (58).
[3] al-Bukhaariy (6094) na Muslim (2607).
- Muhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 161-162
- Imechapishwa: 24/06/2026
Ni muhimu kujua kuwa unafiki umegawanyika aina mbili:
1 – Unafiki wa kiitikadi ambao punde tumetoka kuuzungumzia. Aina hii ya unafiki unamtoa mwenye nao katika Uislamu na mwenye nayo ni miongoni mwa viumbe waovu kabisa.
2 – Unafiki wa kimatendo ambao ni miongoni mwa madhambi makubwa, lakini haumtoi mwenye nao katika Uislamu. Aina hii ndio aliyokusudia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pale aliposema:
”Alama za mnafiki ni tatu; anapoongea anasema uongo, anapoahidi anakhalifu na anapoaminiwa anafanya khiyana.”[1]
Imekuja katika tamko jengine:
“… anapogombana, hufanya uovu…”[2]
Imekuja katika tamko jengine:
“… anapoahidi, anasaliti… “
Hapa kumetajwa alama tatu. Huu ndio unafiki wa kimatendo na ni khatari mno, kwa sababu uwongo unapelekea katika maovu. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Jilazimianeni na ukweli. Hakika ukweli unaongoza katika wema na hakika wema unaongoza katika Peo na mtu ataendelea kusema ukweli mpaka aandikiwe mbele ya Allaah kuwa ni mkweli. Hakika uongo unaongoza katika uovu na uovu unaongoza katika Moto. Hakika mtu ataendelea kusema uongo mpaka aandikwe mbele ya Allaah kuwa ni mwongo.”[3]
Uwongo ni miongoni mwa sifa zinazomchafua muislamu, ni mamoja amesema uwongo juu ya Allaah, Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) au kuwasmea uwongo watu. Namna hii ndivo Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanavyogawanya unafiki. Aina zote mbili mafungu yake yamejulishwa waziwazi ndani ya Qur-aan na Sunnah.
[1] al-Bukhaariy (33) na Muslim (59).
[2] al-Bukhaariy (34) na Muslim (58).
[3] al-Bukhaariy (6094) na Muslim (2607).
Muhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 161-162
Imechapishwa: 24/06/2026
https://firqatunnajia.com/71-aina-mbili-za-unafiki/