Aina ya pili ya watu ni makafiri kama vile waabudia masanamu, mayahudi, manaswara, waabudia moto na wakanamungu. Miongoni mwa sifa zao mbaya ni kwamba hawakuwaitikia Mitume; bali wameipa mgongo ulingano wa Mitume na wafuasi wao:

إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا سَوَاءٌ عَلَيْهِمْ أَأَنذَرْتَهُمْ أَمْ لَمْ تُنذِرْهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ

“Hakika wale waliokufuru ni mamoja kwao ukiwaonya au usiwaonye, wao hawatoamini.”[1]

Baada ya hapo Allaah akabainisha adhabu yao ya duniani na Aakhirah.

Aina ya tatu ya watu ni wanafiki ambao wako na unafiki wa kiimani. Allaah ametaja jinsi wanavyobadilikabadilika, wanadhihirisha kheri, wanaficha shari na kuchukia Uislamu na waislamu. Wale Ahl-ul-Bid´ah ambao wanajifananisha nao ni miongoni mwao katika yale wanayojifananisha nao. Unafiki wa kiitikadi ni mbaya zaidi na unadhuru zaidi Uislamu na waislamu kuliko wale makafiri wenye kuonyesha waziwazi ukafiri wao. Ndio maana adhabu yao ikawa kali zaidi. Kama alivosema Allaah (´Azza wa Jall):

إِنَّ الْمُنَافِقِينَ فِي الدَّرْكِ الْأَسْفَلِ مِنَ النَّارِ وَلَن تَجِدَ لَهُمْ نَصِيرًا

“Hakika wanafiki watakuwa katika tabaka la chini kabisa katika Moto na wala hutompata kwa ajili yao mwenye kunusuru.”[2]

Yule mtenda madhambi anayetubia kwa jumla juu ya madhambi yake, kama vile shirki na madhambi mengine makubwa, Allaah anamsamehe kwa sababu msamaha wa Allaah ni mpana.

[1] 02:06

[2] 04:154

  • Muhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 160
  • Imechapishwa: 24/06/2026