Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) amesema:

Unafiki ni ukafiri na maana yake ni kumkufuru Allaah, kumuabudu mwengine asiyekuwa Yeye na wakati huohuo mtu akaonyesha Uislamu waziwazi. Hivyo ndivyo walivyofanya wanafiki wakati wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

MAELEZO

Mwanzoni mwa Suurah “al-Baqarah” Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) ametaja makundi mbalimbali ya watu, kukiwemo waumini na sifa zao. Miongoni mwa sifa zao ni kama ifuatavyo:

1 – Wanaamini mambo yaliyofichikana, nayo ni yale yote yaliyofichikana machoni mwa mtu.

2 – Wanajitolea matumizi ya wajibu na yanayopendeza katika mali na elimu.

3 – Wanasimamisha swalah kikamilifu.

4 – Wanaamini yale yote yaliyoteremshwa kwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Qur-aan na Sunnah kwa mujibu wa ufahamu wa Salaf.

5 – Wanaamini vile vitabu vyote vilivyoteremshwa na Mitume wote waliyotumilizwa.

6 – Wanaamini siku ya Qiyaamah na yale yote yanayohusiana nayo na yale yote yatayotokea kabla na baada ya kifo.

Hizi ni baadhi ya sifa muhimu za waumini na misingi ya ´Aqiydah yao. Aina ya watu hawa ni wafuasi wa Mitume katika Wahajiri, Wanusuraji na wale waliokuja baada yao hadi siku ya Qiyaamah wanasema:

رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا وَلِإِخْوَانِنَا الَّذِينَ سَبَقُونَا بِالْإِيمَانِ وَلَا تَجْعَلْ فِي قُلُوبِنَا غِلًّا لِّلَّذِينَ آمَنُوا رَبَّنَا إِنَّكَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ

“Mola wetu! Tusamehe sisi na ndugu zetu ambao wametutangulia kwa imani na wala Usijaalie katika nyoyo zetu mafundo kwa wale walioamini – Mola wetu! Hakika ni Mwenye huruma mno, Mwenye kurehemu!”[1]

[1] 59:10

  • Muhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 159-160
  • Imechapishwa: 24/06/2026