Swali: Kuna mtu ameingia msikitini kuswali ´Ishaa kisha akakumbuka kuwa hajaswali Maghrib. Nini anachotakiwa kufanya?
Jibu: Unapoingia msikitini wakati kunapokimiwa ´Ishaa kisha ukakumbuka kuwa hujaswali Maghrib, basi utajiunga na mkusanyiko kwa nia ya kuswali Maghrib. Wakati imamu ataposimama katika Rak´ah ya nne utabaki katika Rak´ah hiyo ya nne, utamsubiri imamu kisha utatoa Tasliym pamoja naye. Unaweza pia kutoa Tasliym kisha ukajiunga na imamu katika ile sehemu ya swalah ya ´Ishaa iliyobakia. Kwa mujibu wa maoni sahihi ya wanazuoni ni kwamba haidhuru kitu kule kutofautiana kwa nia ya imamu na yule anayeswalishwa. Hapana vibaya pia endapo utaswali Maghrib peke yako kisha baadaye ukajiunga na mkusanyiko katika yale utayokuwa umewahi katika swalah ya ´Ishaa.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/221-222)
- Imechapishwa: 23/06/2026
Swali: Kuna mtu ameingia msikitini kuswali ´Ishaa kisha akakumbuka kuwa hajaswali Maghrib. Nini anachotakiwa kufanya?
Jibu: Unapoingia msikitini wakati kunapokimiwa ´Ishaa kisha ukakumbuka kuwa hujaswali Maghrib, basi utajiunga na mkusanyiko kwa nia ya kuswali Maghrib. Wakati imamu ataposimama katika Rak´ah ya nne utabaki katika Rak´ah hiyo ya nne, utamsubiri imamu kisha utatoa Tasliym pamoja naye. Unaweza pia kutoa Tasliym kisha ukajiunga na imamu katika ile sehemu ya swalah ya ´Ishaa iliyobakia. Kwa mujibu wa maoni sahihi ya wanazuoni ni kwamba haidhuru kitu kule kutofautiana kwa nia ya imamu na yule anayeswalishwa. Hapana vibaya pia endapo utaswali Maghrib peke yako kisha baadaye ukajiunga na mkusanyiko katika yale utayokuwa umewahi katika swalah ya ´Ishaa.
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/221-222)
Imechapishwa: 23/06/2026
https://firqatunnajia.com/amekumbuka-kuwa-hajaswali-maghrib-wakati-wa-ishaa/