Ni vipi zinalipwa swalah zilizompita mtu?

Swali: Ni vipi zinalipwa swalah zilizompita mtu?

Jibu: Swalah za faradhi zilizompita mtu zinakidhiwa haraka iwezekanavyo pale kunapoondoka udhuru. Aidha ni wajibu kuziswali kwa mpangilio. Vivyo  hivyo juu ya zile swalah zinazopendeza zilizopangiwa muda maalum, kama vile Witr na zile swalah za Rawaatib.

Kuhusu swalah zinazopendeza zilizoachiwa hazilipwi kwa sababu hazikuwekewa wakati maalum. Mambo yalivyo ni kwamba mtu anaziswali wakati anapotaka pasi po kuwa ndani ya zile nyakati zilizokatazwa.

Swalah zinazopendeza ambazo zinatokana na sababu maalum hazikidhiwi pale kunapoondoka zile sababu zake. Kwa sababu zimefungamana na sababu zake; zinaposwaliwa baada ya sababu zake basi mtu anakuwa hakuziswali kutokana na sababu yake na kwa ajili hiyo hazitakiwi kulipwa.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/222)
  • Imechapishwa: 23/06/2026