68. Wao si kama Khawaarij, wala si kama Raafidhwah

Huu ndio msimamo sahihi. Kwa msemo mwingine haijuzu kufikiria kama Khawaarij wala kufikiria kama Raafidhwah.

Khawaarij wamewakufurisha Maswahabah wengi wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kama vile ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) na jeshi lake, wakawapiga vita na kuhalalisha kumwagwa damu zao.

Raafidhwah wamechupa mipaka kwa watu wa nyumbani kwake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na sambamba na hilo wakaonyesha utovu wa nidhamu kwa Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) wengine waliosalia. Bali wamefikia mpaka kuwakufurisha, khaswa Abu Bakr na ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ambao wanawaita kuwa ni “masanamu mawili ya Quraysh”. Wanawaona Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) waliafikiana juu ya dhambi na mashambulizi na kwamba walikuwa ni wanafiki, kwa sababu eti walifanya usaliti juu ya wasia wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa wasii. Raafidhwah wamesema uwongo na Khawaarij wamepotea. Allaah amewaongoza Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ambao wametambua nafasi na haki za Maswahabah. Upande mmoja hawaoni kuwa wamekingwa na makosa, upande mwingine hawaingilii yale magomvi yaliyotokea baina yao. Wanatambua kuwa Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) ndio ummah bora baada ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wanajua kuwa nafasi na ubora wao unatofautiana. Haya yametamkwa waziwazi ndani ya vitabu vya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah – Allaah avifanye kuwa wingi, awasamehe wafu wao na awanyanyue wale ambao bado wako hai ili wazidi kuwakasirisha Ahl-ul-Bid´ah kwa sampuli zao zote!

  • Muhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 151
  • Imechapishwa: 23/06/2026