Yapuuzieni makosa ya watu wenye kujiheshimu

Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Yapuuzieni makosa ya wenye heshima muda wa kuwa haihusiani na adhabu za kidini.”[1]

Nini maana ya makosa?

Jibu: Ni yule ambaye maovu hayajirudirudi kutoka kwake na wala hatambuliki kwa shari. Ni mwenye kutambulika kujiheshimu na kujichunga na machafu. Hata hivyo baadhi ya nyakati ametumbukia katika makosa ambayo hayapelekei kuadhibiwa. Huyu anasamehewa midhali haihusiani na adhabu za kidini.

[1] Ahmad (25513). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy i “Hadiyyat-ur-Ruwaah” (3/420).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (46)
  • Imechapishwa: 27/07/2024