Ya kwanza ndio faradhi na ya pili ndio sunnah

 Swali: Nilihiji miaka kadhaa iliopita kisha nikajiambiwa mwenyewe kwamba Allaah akinijaalia kuhiji mara zengine basi nitaifanya ile niliohiji mara ya kwanza kuwa sunnah na kunuia hizi za baadaye kuwa ndio faradhi. Kwa sababu wakati wa ile hajj ya kwanza nilikuwa  katika masiku ya ujinga na bado sijajua na utambuzi. Je, inajuzu kwake kufanya hivo?

Jibu: Hajj yake ya faradhi ni ile ya kwanza na hajj ya pili ndio sunnah. Ndugu muislamu! Tambua kuwa sunnah zote zinakamilisha zile faradhi. Sisi tukishamaliza kuswali ´ishaa hivi sasa, ´ishaa iko na sunnah baada yake. Tukiswali Raatibah baada yake, ikiwa faradhi yetu ina kasoro basi Raatibah hii inafuta zile kasoro. Kadhalika huyo mwanamke. Ikiwa hajj yake ya kwanza ina kasoro basi hajj yake ya pili inafuta zile kasoro. Kwani ´ibaadah za faradhi zinakamilishwa na zile ´ibaadah za sunnah siku ya Qiyaamah ikiwa faradhi hizo zilikuwa na mapungufu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (63) http://binothaimeen.net/content/1443
  • Imechapishwa: 28/12/2019