Swali: Ni ipi hukumu ya wudhuu´ kwa wale ambao wanakaa koma/ICU kwa kipindi fulani?

Jibu: Linahitajia upambanuzi; haidhuru ikiwa ni kwa kipindi kifupi kisichoondosha fahamu na wala hakizuii hisia ya kuwepo wudhuu´. Kama mfano wa usingizi wa ambaye halali fofofo katika usingizi wake, bali yuko usingizini lakini anasikia yanayooendelea. Mtu huyu haimdhuru kitu mpaka atambue kuwa ametokwa na kitu. Vivyo hivyo ikiwa kulala koma/ICU hakumzuii hisia. Lakini ikiwa kulala koma/ICU kunamzuia kuhisi yale yanayomtoka, kama vile mlevi au maradhi yaliyomfanya kupoteza fahamu mpaka akalazwa koma/ICU, mtu kama huyu unachenguka wudhuu´ wake kama vile kuzimia. Vivyo hivyo wale ambao wanashikwa na kifafa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/145)
  • Imechapishwa: 13/08/2022