Swali: Naomba kufaidika namna ya kupangusa juu ya soksi na inakuwa kwa mikono miwili yote kwa pamoja au kwa mkono wa kuume au nipangusa mguu wa kuume kwa mkono wa kuume na mguu wa kushoto kwa mkono wa kushoto?

Jibu: Sunnah ni kupangusa mguu wa kulia kwa mkono wa kuume na mguu wa kushoto kwa mkono wa kushoto. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Mtakapotawadha basi anzeni kwa upande wenu wa kuume.”

Wameipokea watunzi wa ”as-Sunan” kwa cheni ya wapokezi Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/107)
  • Imechapishwa: 13/08/2022