Swali: Ninayo tafsiri ya maana ya Qur-aan tukufu kwa lugha ya kingereza. Je, inafaa kafiri kuigusa?

Jibu: Hapana vibaya kafiri kugusa maana ya Qur-aan tukufu kwa lugha ya kingereza au lugha zingine. Tarjama ni tafsiri ya maana ya Qur-aan. Hapana neno kafiri akiigusa au ambaye hana twahara. Kwa sababu tarjama haina hukumu ya Qur-aan. Tarjama ina hukumu ya tafsiri. Hakuna vibaya kwa kafiri na ambaye hana twahara kugusa vitabu vya tafsiri ya Qur-aan. Vivyo hivyo inahusiana na vitabu vya Hadiyth, Fiqh na lugha ya kiarabu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (05/405)
  • Imechapishwa: 13/08/2022