Swali: Kutawadha kwa sababu ya kugusa dhakari endapo mtu atasahau akagusa nyuma ya suruwali?

Jibu: Amegusa ngozi kwa ngozi au nyuma ya suruwali?

Muulizaji: Amegusa ngozi kwa kiasi kidogo.

Jibu: Akigusa ngozi kwa ngozi anatakiwa kutawadha. Ikiwa ni nyuma ya suruwali, nyuma ya nguo au nyuma ya suruwali hapana vibaya. Lakini akigusa ngozi kwa ngozi bi maana akagusa dhakari yake kwa mkono wake basi analazimika kutawadha. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mwenye kugusa dhakari yake basi atawadhe.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21951/ما-حكم-الوضوء-من-مس-الذكر
  • Imechapishwa: 08/10/2022