Swali: Ni yapi mahusiano ya damu? Wakati fulani damu ya mtu kwa mfano inakuwa yenye joto na hivyo nywele zake zinakuwa nyeupe.

Jibu: Hapana. Kitu hicho ni lazima kiwe na sababu. Lakini hatujui sababu zote. Baadhi ya watu mvi zinaweza kuwajilia mapema lakini sababu yake Allaah ndiye anajua upambanuzi wake. Mara nyingi mtu anapokuwa na khofu sana ndipo zinamjilia. Wakati fulani mvi zinaweza kujitokeza kwa sababu ya khofu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21947/هل-لشيب-الشعر-علاقة-بالدم
  • Imechapishwa: 08/10/2022