Swali: Ni wapi imependekezwa Qunuut katika swalah ya Fajr au katika swalah ya Witr? Je, uhakika wa Witr ni kwa sauti ya juu au kimyakimya?

Jibu: Qunuut imependekezwa katika Witr. Kuhusu swalah ya Fajr haikusuniwa kukunuti ndani yake isipokuwa wakati wa majanga. Kwa sababu kilichohifadhi kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kwamba hakufanya hivo isipokuwa wakati wa janga. Haya ndio maoni ya kikosi kikubwa cha wanazuoni na ndio maoni sahihi. Akisoma Qunuut peke yake katika Witr basi atasoma kimyakimya. Akiwa ni imamu basi ataisoma kwa sauti ya juu ili maamuma waitikie ”Aamiyn”.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy

´Abdullaah bin Ghudayyaan

Swaalih al-Fawzaan

´Abdul-´Aziyz Aalish-Shaykh

Bakr Abu Zayd

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.alifta.gov.sa/Ar/IftaContents/Pages/FatawaDetails.aspx?View=Page&PageID=12229&CultStr=ar&PageNo=1&NodeID=1&BookID=3
  • Imechapishwa: 16/04/2022