Je, inafaa kwa mtu kuswali shufwa na witr kwa sauti ya juu?

Swali: Je, inafaa kwa mtu kuswali shufwa na witr kwa sauti ya juu?

Jibu: Inafaa kusoma kwa sauti ya juu na kusoma kimyakimya katika swalah ya shufwa na witr ijapo kusoma kwa suati ya juu ndio bora zaidi muda wa kuwa hamkeri yeyote. Kwa sababu ni sehemu katika swalah ya usiku. Imesuniwa kusoma kwa sauti ya juu katika swalah ya usiku.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy

´Abdullaah bin Ghudayyaan

Swaalih al-Fawzaan

´Abdul-´Aziyz Aalish-Shaykh

Bakr Abu Zayd

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.alifta.gov.sa/Ar/IftaContents/Pages/FatawaDetails.aspx?View=Page&PageID=12226&CultStr=ar&PageNo=1&NodeID=1&BookID=3
  • Imechapishwa: 16/04/2022