Raatibah ya ´Ishaa inaweza kukaa mahali pa shufwa kabla ya Witr?

Swali: Je, inatosha baada ya kumaliza kuswali ´Ishaa mtu akaswali Sunnah ya Raatibah na Rak´ah moja ya Witr peke yake au ni lazima aswali Rak´ah mbili za shufwa pamoja na Witr?

Jibu: Kuswali shufwa kabla ya Witr ndio bora zaidi kuliko mtu kuswali Witr peke yake. Rak´ah mbili za Raatibah ya ´Ishaa hazitoshelezi kutokamana na [Rak´ah mbili za] shufwa. Hata hivyo hapana vibaya kuswali Witr Rak´ah moja.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy

´Abdullaah bin Ghudayyaan

Swaalih al-Fawzaan

´Abdul-´Aziyz Aalish-Shaykh

Bakr Abu Zayd

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.alifta.gov.sa/Ar/IftaContents/Pages/FatawaDetails.aspx?View=Page&PageID=12225&CultStr=ar&PageNo=1&NodeID=1&BookID=3
  • Imechapishwa: 16/04/2022