Amka uswali tena ila usiswali Witr mara ya pili

Swali: Nikiswali ´Ishaa na Tarawiyh katika Ramadhaan na miezi mingine kisha nikaswali Witr kabla ya kulala halafu baadaye nikaamka kwa ajili ya Tahajjud mwishoni mwa usiku – je, nirudie kuswali Witr au nifanye nini kutokana maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Ifanyeni swalah yenu ya mwisho usiku ni Witr.”?

Jibu: Haikusuniwa kwako kurudia kuswali Witr kutokana na Hadiyth isemayo:

“Hakuna Witr mbili katika usiku mmoja.”

Ukitaka kuswali sunnah inafaa kwako kufanya hivo lakini bila kurudia Witr tena.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy

´Abdullaah bin Ghudayyaan

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.alifta.gov.sa/Ar/IftaContents/Pages/FatawaDetails.aspx?View=Page&PageID=12223&CultStr=ar&PageNo=1&NodeID=1&BookID=3
  • Imechapishwa: 16/04/2022