Wingi na uchache wa Rak´ah za Rawaatib

Swali: Ni jambo limethibiti katika Sunnah ya kwamba Rawaatib ni Rak´ah kumi na nne?

Jibu: Rawaatib uchache wake ni Rak´ah kumi: Rak´ah mbili kabla ya Fajr, Rak´ah mbili kabla ya Dhuhr, Rak´ah mbili baada ya Dhuhr, Rak´ah mbili baada ya Maghrib na Rak´ah mbili baada ya ´Ishaa.

Rawaatib wingi wake ni Rak´ah kumi na nne: Rak´ah mbili kabla ya Fajr, Rak´ah nne kabla ya Dhuhr, Rak´ah mbili baada ya Dhuhr, Rak´ah mbili baada ya Maghrib na Rak´ah mbili baada ya ´Ishaa.

Huu ndio wingi wake na uchache wake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/liqo%20%20-%2021%20-%2008%20-%201435.mp3
  • Imechapishwa: 09/04/2015