Wewe usiwe wa kwanza kumsalimia kafiri

Swali: Ni ipi hukumu ya mtu kuanza kumsalimia kafiri?

Jibu: Haijuzu. Ni haramu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Msianze kuwapa mayahudi na manaswara salamu. Wakikusalimieni waambieni: “Nanyi pia.” Ibn Maajah (2999). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy.

Swali: Inajuzu kuanza kumsalimia kafiri kwa isiyokuwa salamu kama kumwambia “Khabari ya asubuhi?”

Jibu: Huku pia ni kumsalimia hata kama matamshi yatatofautiana. Wewe usianze kumsalimia. Lakini yeye akianza kukusalimia na wewe muitikie.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (03) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/omdah–14340316.mp3
  • Imechapishwa: 25/08/2020