Wenye kuwajibika na wasiowajibika kumpokea mgeni

Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

15 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Anayemwamini Allaah na siku ya Mwisho azungumze [mambo ya] kheri au anyamaze; na yule anayemwamini Allaah na siku ya Mwisho amkirimu jirani yake; na yule anayemwamini Allaah na siku ya Mwisho amkirimu mgeni wake.”

Ni wajibu kumkirimu mgeni kwa kumlisha, kama inavyofahamisha Hadiyth hii, kwa muda wa mchana mmoja na usiku wake kwa kumpa yale anayohitajia. Wanachuoni wamesema hili linahusiana na wale watu wa vijiji ambapo hakuna nyumba za kuwapangia wageni. Kuhusiana na miji mikubwa ambayo ina nyumba za kupanga, si wajibu kumpokea mgeni kwa kuwa hawezi kupotea. Isipokuwa ikiwa kama ni mwenye kuhitajia hilo na hana mahali pa kufikia. Katika hali hii itakuwa ni wajibu kwa baadhi ya watu kumsimamia na kumpokea kwa mchana mmoja na usiku wake. Kutimiza siku tatu ni jambo limependekezwa. Hili linahusiana na mahali ambapo hakuna nyumba za kumpangia. Kwa mfano leo katika miji mikubwa, sio wajibu. Ni jambo limependekezwa tu. Ama katika vijiji vidogo vidogo ni wajibu kwa watu wa mji huo kuwapokea wageni wanapowajia kwa muda wa mchana mmoja na usiku wake. Ugeni unatimia kwa muda wa michana mitatu na nyusiku zake.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 245
  • Imechapishwa: 14/05/2020