Wenye kusoma shairi la al-Burdaa hawana tofauti na wanavyofanya manaswara      

Swali: Kuna mmoja katika Suufiyyah anasema akitetea Qaswiydah yao inayomsifu Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Msinisifu kwa kipindukia kama walivyopetuka manaswara kwa mwana wa Maryam.”

manaswara walisema kuwa al-Masiyh ni mwana wa Allaah na sisi hatukusema hivo katika Qaswiydah yetu. Vipi kumraddi?

Jibu: Ukimuomba Mtume na kutaka uokozi kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) basi wewe ni kama mnaswara. Wenye kusema maneno hayo[1] wanamuomba msaada Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na uokozi wakati wa majanga. Bali hata waabudu makaburi wanamnadi na kumuomba uokozi na huku wanasema kuwa hawakufanya kama walivyofanya manaswara. Haya ndio matendo ya manaswara. Kumshirikisha Allaah ndio matendo ya manaswara. Huku ndio kumshirikisha Allaah (´Azza wa Jall). Unataka kusema kuwa shirki haiwi isipokuwa tu yale yenye kufanywa na manaswara peke yake?

[1] Mtunzi wa al-Burdaa al-Buuswayriy amesema:

“Ewe kiumbe bora – yaani Mtume! Ni nani mimi nitamkimbilia kutaka aniokoe tukio kubwa la Qiyaamah litapofika. Ikiwa [siku hiyo] hutonishika mkono basi nitaanguka na kuangamia. Hakika kwa utukufu na fadhila zako ndio maana dunia na Akhera vikawepo na katika elimu yako unajua mpaka elimu iliyoko katika ubao Uliyohifadhiwa.” (al-Burdaa)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (09) http://alfawzan.af.org.sa/node/2127
  • Imechapishwa: 05/07/2020