Msimamo wa wanafunzi kwa nyujumbe za makhurafi

Swali: Baadhi ya watu siku hizi wanaeneza nyujumbe kwa njia ya simu zinazotoka kwa mtu anayeitwa ´Abdullaah. Mtu huyu anasema kuwa amemshuhudia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa macho yake usingizini na akamuusia awasalimie watu na mwenye kusoma ujumbe huo aueneze na asubiri siku nne ambapo atafurahi furaha iliokuwa kubwa na asiyeueneza ujumbe huo atapata huzuni uliokuwa mkubwa. Ni ipi nasaha yako kwa kitu kama hiki?

Jibu: Huyu ni mwongo. Uongo wake uko wazi katika jambo hili. Hili liko wazi kabisa. Kule kusema tu kuwa amemuona Mtume… Ni kweli yawezekana kuwa amemuona kweli au hakumuona. Lakini kusema na kuweka kiwango cha siku nne kwa mwenye kueneza ujumbe huo kupata kitu kadhaa na kwamba asiyeueneza atapata huzuni, huku ni kumsemea uongo Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mfano wa ukhurafi kama huu ni wajibu ukemewe na wanafunzi wamraddi huyo muenezaji kwenye simu hiyo hiyo. Wanatakiwa kumraddi muenezaji kwenye simu hiyo hiyo mpaka watu hawa wakome.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (09) http://alfawzan.af.org.sa/node/2127
  • Imechapishwa: 05/07/2020