Wazazi makafiri hawataki msichana wao afanye Hijrah na aolewe

Swali: Mwanamke huyu ni wa kutoka Ujerumani amesilimu na anataka kuolewa na kufanya Hijrah katika nchi hii. Lakini wazazi wake ambao ni makafiri hawataki hayo. Je, awatii katika hilo?

Jibu: Asiwatii katika hayo. Asiwatii katika kumuasi Allaah; si katika kuacha Hijrah wala kuacha kuolewa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (55) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-11-10.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020