Swali 233: Ni ipi hukumu kwa mwenye kuswali yeye na mke wake kwa kutumia Siwaak moja? Je, kitu hicho kinajuzu?
Jibu: Hapana neno. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika maradhi aliyokufia, kama ilivyo katika Hadiyth ya ´Aaishah, ´Abdur-Rahmaan bin Abiy Bakr aliingia kwake ambapo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawa anamtazama. Ndipo ´Aaishah akatambua kuwa anachotaka ni Siwaak. Akamuomba ´Abdur-Rahmaan ampe Siwaak. Akaichukua, akaitafunatafuna, akausafisha halafu akampa nao Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Amesema katika Hadiyth maneno yenye maana ifuatayo: yakachanganyikana mate yangu na mate yake katika jambo lake la mwisho. Vivyo hivyo mtu kwa mtu mwengine ikiwa haoni vibaya. Ikiwa anaona vibaya kutoka kwa ndugu yake hakuna neno na wala mtu halaumiwi. Kwani watu wanatofautiana. Ikiwa anaona vibaya hakuna neno na wala halaumiwi.
- Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ijaabatu as-Saa-il, uk. 450
- Imechapishwa: 29/10/2019
Swali 233: Ni ipi hukumu kwa mwenye kuswali yeye na mke wake kwa kutumia Siwaak moja? Je, kitu hicho kinajuzu?
Jibu: Hapana neno. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika maradhi aliyokufia, kama ilivyo katika Hadiyth ya ´Aaishah, ´Abdur-Rahmaan bin Abiy Bakr aliingia kwake ambapo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawa anamtazama. Ndipo ´Aaishah akatambua kuwa anachotaka ni Siwaak. Akamuomba ´Abdur-Rahmaan ampe Siwaak. Akaichukua, akaitafunatafuna, akausafisha halafu akampa nao Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Amesema katika Hadiyth maneno yenye maana ifuatayo: yakachanganyikana mate yangu na mate yake katika jambo lake la mwisho. Vivyo hivyo mtu kwa mtu mwengine ikiwa haoni vibaya. Ikiwa anaona vibaya kutoka kwa ndugu yake hakuna neno na wala mtu halaumiwi. Kwani watu wanatofautiana. Ikiwa anaona vibaya hakuna neno na wala halaumiwi.
Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ijaabatu as-Saa-il, uk. 450
Imechapishwa: 29/10/2019
https://firqatunnajia.com/watu-wawili-kutumia-siwaak-moja/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)