Kunyoa ndevu ni kujifananisha na wanawake na ni kujifananisha na makafiri. Kilicho dhahiri ni kwamba wa mwanzo waliowawekea waislamu mwenendo huu mbaya ni Suufiyyah, kama ilivyotajwa katika “Talbiys Ibliys”. Allaah ameupa mtihani Uislamu kwa Suufiyyah na Shiy´ah.
Kupunguza urefu wake na upana wake ni jambo halikuthibiti. Kwa hiyo ziache ndevu zako na zifuge, kama alivyoamrisha Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ndevu zimetajwa mpaka kwenye Qur-aan pale ambapo Haaruun aliposema:
يَا ابْنَ أُمَّ لَا تَأْخُذْ بِلِحْيَتِي وَلَا بِرَأْسِي ۖ إِنِّي خَشِيتُ أَن تَقُولَ فَرَّقْتَ بَيْنَ بَنِي إِسْرَائِيلَ وَلَمْ تَرْقُبْ قَوْلِي
“Ee mwana wa mama yangu! Usinishike ndevu zangu na wala kichwa changu. Hakika mimi niliogopa usije kusema “Umefarikisha kati ya wana wa Israaiyl na wala hukuchunga kauli yangu.”[1]
[1] 20:94
- Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ijaabatu as-Saa-il, uk. 219
- Imechapishwa: 26/09/2019
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)