Swali: Je, Aakhirah watu watajuana kama jinsi walivyokuwa wakijuana duniani?

Jibu: Bila ya shaka Aakhirah watajuana kati yao:

وَيَوْمَ يَحْشُرُهُمْ كَأَن لَّمْ يَلْبَثُوا إِلَّا سَاعَةً مِّنَ النَّهَارِ

“Na [wakumbushe] Siku atakayowakusanya [wataona] kama kwamba hawakuishi [duniani] isipokuwa saa moja ya mchana.” (10:45)

Watajuana kati yao. Watajuana wao kwa wao. Baba atamjua mtoto wake na mtu atamjua kaka yake. Lakini hakuna yeyote ataweza kumsaidia mwenzie:

يَوْمَ يَفِرُّ الْمَرْءُ مِنْ أَخِيهِ

“Siku mtu atakapomkimbia ndugu yake.” (80:34)

يُبَصَّرُونَهُمْ ۚ يَوَدُّ الْمُجْرِمُ لَوْ يَفْتَدِي مِنْ عَذَابِ يَوْمِئِذٍ بِبَنِيهِ

“Watafanywa waonane, [lakini] mhalifu atatamani ajikomboe na adhabu siku hiyo kwa [kuwatoa] watoto wake.” (70:11)

Watafanywa waonane kati yao. Haina shaka yoyote kuwa watajuana. Lakini hata hivyo hakuna yeyote ataweza kumsaidia mwenzie katika kisimamo hicho na siku hiyo. Kila mmoja atakuwa ni mwenye kushughulishwa na matendo yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (49) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-6-3.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020