Swali: Kuna wanaosema mtu asisome vitabu vya Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah na vitabu vya Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab kwa hoja ya kwamba watu wanakimbia kutokana na majina ya waandishi hawa na badala yake mtu asome vitabu vingine kuhusu ´Aqiydah. Kwa mfano vitabu vya Shaykh Haafidhw al-Hakamiy au vitabu vipya vya baadhi ya waandishi wa sasa. Ni upi usahihi juu ya jambo hili?

Jibu: Haafidhw al-Hakamiy (Rahimahu Allaah) vitabu vyake amevitoa wapi? Hakuviandika isipokuwa kutoka kwenye vitabu vya Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah na vitabu vya Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab. Hakujitolea kitu kwa mujibu wake.

Mwenye kukimbia jina la Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah au jina la Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab, huyu hataki haki. Majina haya yana dhambi gani? Hii ni dalili inayoonesha kuwa mtu huyu hajui mfumo wao, ulinganizi wao na yale waliyokuwemo. Makusudio yake sio jina peke yake. Haya ni maneno ya kuoza na yapuuzwe.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (17) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1427-11-6.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2020