Wanawake waliokufa kabla ya kuolewa Peponi  

Swali: Wanawake ambao hawakuolewa duniani watakuwa na nani Peponi? Je, watakuwa na waume?

Jibu: Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

إِنَّا أَنشَأْنَاهُنَّ إِنشَاءً فَجَعَلْنَاهُنَّ أَبْكَارًا عُرُبًا أَتْرَابًا لِّأَصْحَابِ الْيَمِينِ

“Hakika Sisi tunawaanzisha [al-Huur al-´Aiyn] uanzishaji. Tunawafanya mabikra. Wenye mahaba kwa waume zao, hirimu moja. Kwa ajili ya watu wa kuliani.” (56:35-38)

Wanawake hawa siku ya Qiyaamah watarudi kuwa mabikira baada ya duniani kuwa wazee. Wataozeshwa watu wa Peponi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (17) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1427-11-6.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2020