Waswaliji wafanye nini imamu anapotoa salamu kwa Rak´ah pungufu?

Swali: Imamu akitoa salamu kwa upungufu na maamuma wana uhakika kuwa ametoa salamu kwa upungufu – je, watoe salamu pamoja naye?

Jibu: Hapana, wasitoe salamu. Wamkumbushe kwa kusema:

سبحان الله

“Allaah ametakasika kutokana na mapungufu.”

Swali: Kipi kinachomlazimu imamu asipozinduka? Je, mtu ajitolee kumzungumzisha?

Jibu: Hapana, atajua. Waswaliji wakisema:

سبحان الله

“Allaah ametakasika kutokana na mapungufu.”

atajua.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23600/ما-يفعل-الماموم-لو-سلم-الامام-عن-نقص
  • Imechapishwa: 23/02/2024