Waswaliji kusimama wanapomuona imamu ameingia msikitini

Swali: Waswaliji husimama pale tu wanapomuona imamu ameingia mlango wa msikiti.

Jibu: Ikiwa desturi ya imamu ni kwamba anapoingia ndio hukimiwa swalah, basi wasisimame mpaka kukimiwe swalah ingawa wamemuona ameingia. Kwa sababu Bilaal alikuwa anapomuona (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameingia hukimu swalah. Lakini wakati mwingine anaweza kukimu kabla ya imamu kuingia kwa mujibu wa miadi iliopo baina yake na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)… Kwa hivyo wasisimame mpaka wamemuona imamu ameingia.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23710/حكم-قيام-المامومين-عند-دخول-الامام-المسجد
  • Imechapishwa: 07/04/2024