Sunnah ya Dhuhr pindi joto ni kali

Swali: Mwenye kutaka kuchelewesha swalah, mbali na Dhuhr, bora aadhini pamoja na misikiti mingine ndani ya wakati kisha aswali pale itapombainikia?

Jibu: Ndio, aadhini pamoja na misikiti mingine. Inategemea na swalah yenyewe. Kwa mfano inapokuja katika ´Ishaa; akiona wamekuja mapema huitanguliza, na akiona wamechelewa huichelewesha.

Swali: Dhuhr peke yake ndio inacheleweshwa adhaana na swalah?

Jibu: Joto likiwa kali wacheleweshe adhaana na swalah. Hiyo ndio Sunnah.

Swali: Kwa maana nyingine hilo ni jambo maalum kwa ajili ya Dhuhr, kwa isiyokuwa Dhuhr mtu aadhini ndani ya wakati?

Jibu: Ndio.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23708/هل-يوذن-في-الوقت-بمسجد-يوخر-الصلاة
  • Imechapishwa: 07/04/2024