Wasiwasi wa kutokwa na mkojo baada ya kukidhi haja ndogo

Swali: Mtu afanye nini mkojo ukimchosha akitokwa na tone punde tu baada ya kutoka bafuni mara moja au mara mbili na hajui kama ni wasiwasi?

Jibu: Mimi nachelea ikawa ni wasiwasi wa muulizaji. Dawa ya wasiwasi ni kutounyenyekea. Ni lazima uinuke, usubiri na utazame. Ikiwa ni wasiwasi basi pengine ikaondoka hali hiyo kwa kuipuuza. Ikiwa kweli imetokea, unapomaliza kukojoa ikiwa kukidhi kwako haja ndogo kutachukua muda mrefu basi weka bendeji juu ya uume wako, tawadha na uswali kutegemea hali yako hata kama mkojo utakutoka wakati uko unaswali.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.mufti.af.org.sa/ar/content/مالحكم-إذا-خرج-من-الشخص-قطرة-أو-قطرتين-من-البول-بعد-قضاءه-لحاجته
  • Imechapishwa: 12/06/2022