Kuingia chooni na simu iliyo na msahafu na mwenye janaba kugusa simu yenye Qur-aan

Swali: Je, inafaa kuingia chooni na mfukoni mwangu kuna na simu ilio na Qur-aan na Adhkaar? Je, inafaa kugusa na kubeba simu hiyo kwa ambaye yuko na janaba pamoja na kuzingatia kwamba ndani yake kuna msahafu mzima?

Jibu: Hapana neno ikiwa simu imezimwa na haikuwashwa. Ni kama mfano wa kanda. Lakini ikiwa simu imewashwa basi haisilihi. Kwa sababu si sawa kusoma Qur-aan chooni na bafuni. Lakini ikiwa imezimwa hakuna neno kufanya hivo.

Haidhuru kwa mwenye janaba kushika simu ilio ndani msahafu. Kwa sababu Qur-aan iliyomo ndani kilugha haiitwi kuwa ni msahafu.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.mufti.af.org.sa/ar/content/حكم-الدخول-بالجوال-الذي-فيه-القرآن-أو-الأذكار-إلى-دورة-المياه
  • Imechapishwa: 12/06/2022