Wasiomkufurisha mwenye kuswali ni watu wa Bid´ah?

Swali: Je, wale wanaosema kwamba kuacha swalah ni kufuru ndogo na sio kubwa inayomdumisha mwenye nayo Motoni ni watu wa Bid´ah?

Jibu: Hapana, sio watu wa Bid´ah. Haya yamesemwa na baadhi ya wanachuoni na maimamu. Lakini hata hivyo ni makosa. Dalili sahihi zinaonyesha makosa ya kauli hii pasi na kujali aliyeisema. Lakini haifikii kiasi cha kukufurishwa au kuritadishwa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (19) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1427-11-20.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2020