Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kuacha kuswali Fajr ilihali anamsikia muadhini akisema “Swalah ni bora kuliko usingizi”?
Jibu: Ilitakikana kwa muulizaji kuuliza hukumu ya mwenye kuacha swalah ya mkusanyiko ilihali anamsikia muadhini akisema “Njooni katika swalah” ili ikusanye swalah ya Fajr na swalah nyenginezo. Isitoshe sentesi “Njooni katika swalah” ni nzito zaidi kuliko sentesi “Swalah ni bora kuliko usingizi” na sababu nyingine hiyo jumla ya kwanza sio nguzo katika adhaana tofauti na hiyo jumla ya pili ambayo ni nguzo yake.
Kwa hali yoyote haijuzu kwa mwanamme yeyote anayemsikia muadhini anaita kuja kuswali akabaki nyuma isipokuwa kama yuko na udhuru unaokubalika katika Shari´ah. Ibn Umm Maktuum (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
”Nilisema: ”Mtume wa Allaah! Sina kiongozi wa kuniongoza msikitini na mimi ni kipofu. Je, ninayo ruhusa ya kuswali nyumbani kwangu?” Akamuuliza (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Je, wasikia wito wa swalah?” Akasema: “Ndio.” Akasema: “Basi imewajibika.”[1]
Hii ni dalili ya wazi kabisa ya kwamba kila ambaye anamsikia muadhini basi ni lazima kwake kumuitikia.
[1] Muslim (653) na Abu Daawuud (552) ambaye tamko lake limekusanywa.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/37)
- Imechapishwa: 29/04/2026
Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kuacha kuswali Fajr ilihali anamsikia muadhini akisema “Swalah ni bora kuliko usingizi”?
Jibu: Ilitakikana kwa muulizaji kuuliza hukumu ya mwenye kuacha swalah ya mkusanyiko ilihali anamsikia muadhini akisema “Njooni katika swalah” ili ikusanye swalah ya Fajr na swalah nyenginezo. Isitoshe sentesi “Njooni katika swalah” ni nzito zaidi kuliko sentesi “Swalah ni bora kuliko usingizi” na sababu nyingine hiyo jumla ya kwanza sio nguzo katika adhaana tofauti na hiyo jumla ya pili ambayo ni nguzo yake.
Kwa hali yoyote haijuzu kwa mwanamme yeyote anayemsikia muadhini anaita kuja kuswali akabaki nyuma isipokuwa kama yuko na udhuru unaokubalika katika Shari´ah. Ibn Umm Maktuum (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
”Nilisema: ”Mtume wa Allaah! Sina kiongozi wa kuniongoza msikitini na mimi ni kipofu. Je, ninayo ruhusa ya kuswali nyumbani kwangu?” Akamuuliza (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Je, wasikia wito wa swalah?” Akasema: “Ndio.” Akasema: “Basi imewajibika.”[1]
Hii ni dalili ya wazi kabisa ya kwamba kila ambaye anamsikia muadhini basi ni lazima kwake kumuitikia.
[1] Muslim (653) na Abu Daawuud (552) ambaye tamko lake limekusanywa.
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/37)
Imechapishwa: 29/04/2026
https://firqatunnajia.com/wasikia-muadhini/