Swali: Sisi tunasoma katika nchi ya kikafiri ambayo haina ambao wanastahiki kupewa zakaah ya mali au Zakaat-ul-Fitwr. Je, inafaa inafaa kuwapa kituo cha Kiislamu ambacho kinataka kujengwa?
Jibu: Ufumbuzi wa tatizo hili ni mwepesi. Mnaweza kumuwakilisha mtu ima katika mji yenu, au katika nchi nyingine ambayo ina wale watu wanaostahiki kupewa zakaah.
Haijuzu kuwapa zakaah makao makuu ya Kiislamu ambayo yanataka kujengwa. Kwa sababu kituo cha Kiislamu sio miongoni mwa zile aina za wanaopewa zakaah. Makusudio ya kutoa zakaah katika njia ya Allaah kunakusudiwa kupambana jihaad katika njia ya Allaah. Hayo ndio maoni ya wanazuoni wengi. Makusudio sio ueneaji wa manufaa, kama wanavosema baadhi ya watu waliokuja nyuma. Mambo yangelikuwa hivo, basi kusingelikuwa na maana ya kuifanyia zakaah kikomo katika yale makundi manane katika Aayah:
إِنَّمَا الصَّدَقَاتُ لِلْفُقَرَاءِ وَالْمَسَاكِينِ وَالْعَامِلِينَ عَلَيْهَا وَالْمُؤَلَّفَةِ قُلُوبُهُمْ وَفِي الرِّقَابِ وَالْغَارِمِينَ وَفِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَابْنِ السَّبِيلِ ۖ فَرِيضَةً مِّنَ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ
“Hakika si venginevyo zakaah ni kwa ajili ya mafakiri na masikini na wanaozitumikia na wanaotiwa nguvu nyoyo zao [kwa ajili ya Uislamu] na kuwakomboa mateka na wenye deni na katika njia ya Allaah na msafiri [aliyeharibikiwa] – ni faradhi itokayo kwa Allaah; na Allaah ni Mjuzi, Mwenye hekima.”[1]
[1] 09:60
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/317)
- Imechapishwa: 28/04/2026
Swali: Sisi tunasoma katika nchi ya kikafiri ambayo haina ambao wanastahiki kupewa zakaah ya mali au Zakaat-ul-Fitwr. Je, inafaa inafaa kuwapa kituo cha Kiislamu ambacho kinataka kujengwa?
Jibu: Ufumbuzi wa tatizo hili ni mwepesi. Mnaweza kumuwakilisha mtu ima katika mji yenu, au katika nchi nyingine ambayo ina wale watu wanaostahiki kupewa zakaah.
Haijuzu kuwapa zakaah makao makuu ya Kiislamu ambayo yanataka kujengwa. Kwa sababu kituo cha Kiislamu sio miongoni mwa zile aina za wanaopewa zakaah. Makusudio ya kutoa zakaah katika njia ya Allaah kunakusudiwa kupambana jihaad katika njia ya Allaah. Hayo ndio maoni ya wanazuoni wengi. Makusudio sio ueneaji wa manufaa, kama wanavosema baadhi ya watu waliokuja nyuma. Mambo yangelikuwa hivo, basi kusingelikuwa na maana ya kuifanyia zakaah kikomo katika yale makundi manane katika Aayah:
إِنَّمَا الصَّدَقَاتُ لِلْفُقَرَاءِ وَالْمَسَاكِينِ وَالْعَامِلِينَ عَلَيْهَا وَالْمُؤَلَّفَةِ قُلُوبُهُمْ وَفِي الرِّقَابِ وَالْغَارِمِينَ وَفِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَابْنِ السَّبِيلِ ۖ فَرِيضَةً مِّنَ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ
“Hakika si venginevyo zakaah ni kwa ajili ya mafakiri na masikini na wanaozitumikia na wanaotiwa nguvu nyoyo zao [kwa ajili ya Uislamu] na kuwakomboa mateka na wenye deni na katika njia ya Allaah na msafiri [aliyeharibikiwa] – ni faradhi itokayo kwa Allaah; na Allaah ni Mjuzi, Mwenye hekima.”[1]
[1] 09:60
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/317)
Imechapishwa: 28/04/2026
https://firqatunnajia.com/zakaah-katika-kituo-cha-kiislamu-kwenye-nchi-ya-kikafiri/