Amekwama kwenye msongamano wa gari wakati muda wa swalah unataka kuisha

Swali: Umesema katika fatwa yako iliyotangulia ya kwamba ikiwa mwenye kuhiji anakhofia kutoka kwa wakati wa swalah, basi analazimika kutoka nje ya gari na kuswali. Kipi afanye ikiwa hawezi kushuka kwa sababu ya msongamano na gari iko inatembea?

Jibu: Ikiwa hawezi kushuka basi ataswali ijapo ni ndani ya chombo chake cha usafiri. Allaah (Ta´ala) amesema:

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ

”Mcheni Allaah muwezavyo.”[1]

Hata hivyo nafikiria kwamba kuna uwezekano wa yeye kuweza kushuka katika hali hii. Kwa sababu kuna uwezekano daima wa kuegesha gari kando na kuswali. Kwa hali yoyote haijuzu kwa mtu yeyote kuchelewesha Maghrib na ´Ishaa mpaka ukatoka wakati wa Maghrib na ´Ishaa kwa hoja eti anataka kutekeleza Sunnah na hivyo asiswali isipokuwa Muzdalifah. Ucheleweshaji wake huu ni kwenda kinyume na Sunnah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alizichelewesha, lakini aliziswali ndani ya nyakati zake.

[1] 64:16

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/206)
  • Imechapishwa: 29/04/2026