Wasia wa kuzikwa karibu na mtu fulani

Swali: Baadhi ya watu wanaacha wasia wazikwe karibu na waalimu zao au mababu zao wema. Ni ipi hukumu ya kitendo hichi na wasia utekelezwe?

Jibu: Sio lazima. Azikwe na waislamu popote pale. Ikiwa anakusudia kusafirishwa kutoka katika mji wa kikafiri na kupelekwa katika mji wa Kiislamu, ni sawa. Hili ni lengo zuri. Lakini hata katika miji ya makafiri kuna makaburi ya waislamu. Asli ni kuwa mtu anazikwa pamoja na waislamu wenzake popote pale. Lakini ikiwa ndio pendekezo lake na hakuna uzito wa kusafirishwa, asafirishwe.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (19) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf%2030-7-1434_01.mp3
  • Imechapishwa: 15/06/2020