Mtu anaswali Maghrib kwa mara ya pili

Swali: Baada ya kuswali Maghrib niliona mtu mwingine amesimama mwenyewe akiswali Maghrib na nikawa nimependelea kuswali pamoja naye. Je, nitoe Tasliym pamoja naye au nizidishe Rakaa´ ya nne?

Jibu: Sijui dalili yoyote ya kwamba unatakiwa uzidishe Rakaa´ ya nne. Swali na utoe Tasliym naye.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (19) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf%2030-7-1434_01.mp3