Mwanafunzi katika mji ulio na kaburi lililojengewa

Swali: Mwanafunzi anatakiwa kuchukua msimamo upi ikiwa katika mji wake kuna kaburi lililojengewa?

Jibu: Anatakiwa kulingania katika dini ya Allaah na kubainisha kuwa ni shirki na haijuzu. Anatakiwa kubainisha na kukariri nasaha zake. Huenda Allaah akawanufaisha kwazo. Asiwaache watu, akaonelea kuwa hakuna faida yoyote na akanyamaza ilihali anaweza kubainisha, kutoa nasaha na kueneza elimu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (19) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf%2030-7-1434_01.mp3
  • Imechapishwa: 15/06/2020