Wanyama wanaochinjwa kwa mshtuko wa umeme

Swali: Baadhi ya nchi huchinja kuku kwa mshtuko wa umeme au kwa kunyonga. Mtu afanye nini ikiwa hapati njia nyingine isipokuwa hiyo? Je, anaweza kula nyama hiyo?

Jibu: Hapana, hiyo ni amekufa mwenyewe.

Swali: Je, ni lazima mtu awe na uhakika wa jambo hili?

Jibu: Ikiwa ni kutoka kwa wanyama waliyochinjwa na watu wa Kitabu, basi inajuzu kula, isipokuwa iwapo itathibitika kwake kwamba wamechinja kinyume na Shari´ah ya Kiislamu, kama vile kwa mshtuko wa umeme au njia nyingine isiyohalali. Lakini ikiwa ni kutoka kwa wanyama waliyochinjwa na waabudia moto au washirikina, basi inaharamika kabisa.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25324/حكم-الاكل-مما-ذبح-بالصعق-او-الخنق
  • Imechapishwa: 25/02/2025