Swali: Baadhi ya madaktari wa macho wanadai kuwa uwanja unayadhuru macho na wanashauri kutotumia. Ni kipi unachowaambia?

Jibu: Uwanja aina ya (الإثمد) unatambulika kwamba ni mzuri na unayanufaisha macho. Hata hivyo sijui lolote juu ya aina nyenginezo za wanja. Hata hivyo madaktari waaminifu ndio wanaorejelewa katika jambo hili.

Inasemekana kwamba wakati Zarqaa’ al-Yamaamah, ambaye alikuwa akitambulika kwa kuona kwake kukali, wakati alipouliwa waligundua kuwa machoni mwake alikuwa amepaka wanja aina hii ya (الإثمد). Hii leo kuna aina nyingi ya wanja wanazojipaka wanawake. Wanawake wanatumia pensili za kivuli cha macho ambazo hatujui zimetengenezwa kwa kitu gani. Kuna uwezekano zimetengenezwa na mafuta ya nguruwe au mbaya zaidi. Naona kuwa suala hili ni muhimu na kuna umuhimu liandikiwe ukaguzi wenye faida.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/53)
  • Imechapishwa: 16/05/2026