Swali: Kumeshapita miaka tano au sita sijaona familia yangu na wala wao hawajaniona. Je, napata dhambi ikiwa nitajipiga picha na kuwatumia picha?

Jibu: Kujichukua picha kwa lengo hili ni haramu na wala haijuzu, kwa sababu kuhifadhi picha kwa ajili ya kumbukumbu ni haramu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Malaika hawaingii ndani ya nyumba yenye picha.”[1]

Pale ambapo Malaika hawaingii hakuna kheri ndani yake. Unachoweza ni kuwapigia simu familia yao, jambo ambalo litawapa utulivu zaidi juu ya uzima wako kuliko kutumiana picha.

[1] al-Bukhaariy na Muslim.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/354)
  • Imechapishwa: 16/05/2026