Kuangusha deni na kuizingatia kuwa ni zakaah

Swali: Kuna bwana mmoja amemkopesha mwingine kiwango fulani cha pesa. Baada ya kipindi fulani mkopeshwa akaaga dunia na hakuacha isipokuwa nyumba moja tu wanayoeshi ndani yake watoto hawa wadogo. Mkopesha hajalipwa pesa yake. Je, inafaa kwake kufuta deni hili au sehemu yake na badala yake akaizingatia kuwa ni katika zakaah?

Jibu: Haijuzu kwa mkopesha kuangusha deni lake na akanuia kuwa ndio zakaah yake.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/381)
  • Imechapishwa: 16/05/2026