Swali: Unasemaje juu ya ambaye anasema kuwa wanawake hawatomuona Allaah siku ya Qiyaamah?

Jibu: Ni kosa. Allaah ataonekana na waumini wote wa kiume na waumini wote wa kike. Wote watamuona Allaah siku ya Qiyaamah na ndani ya Pepo. Hii ndio neema kubwa zaidi ya watu wa Peponi. Amesema (´Azza wa Jall):

لِّلَّذِينَ أَحْسَنُوا الْحُسْنَىٰ وَزِيَادَةٌ

“Kwa wale waliofanya wema watapata mazuri kabisa na ziada.” (10:26)

Imethibiti kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba maana ya “ziada” ni kutazama uso wa Allaah na maana ya “wema” ni Pepo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema tena katika Hadiyth Swahiyh wakati Maswahabah walipomuuliza: “Je, tutamuona Mola wetu?” Akasema: “Je, kwani nyinyi mnasongamana katika kutazama jua mchana kweupee pasipo mawingu?” Wakasema: “Hapana, ee Mtume wa Allaah.” Akawauliza tena: “Je, kwani nyinyi mnasongamana katika kutazama mwezi usiku wenye mwezi kamili ukiwa waziwazi pasipo mawingu?” Wakasema: “Hapana, ee Mtume wa Allaah.” Ndipo akasema: “Basi vivyo hivyo ndivo mtamuona Mola wenu kama mnavoona mwezi na jua.”

Hili ni lenye kuenea kwa wanamme na wanawake wote. Ni miongoni mwa neema nao wanawake ni wenye kushirikiana na wanamme katika neema. Wanamme na wanawake ni wenye kushirikiana katika neema. Hii pia ni neema. Bali ndio neema kubwa zaidi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/4400/حكم-زعم-ان-النساء-لا-يرين-الله-في-القيامة
  • Imechapishwa: 17/06/2022