Wanaume wanaovaa mavazi mepesi yenye kuonyesha ndani

Swali: Ambaye anaonesha viungo kwa wepesi kupitia ndani yake, je, kuna neno lenye athari katika nyoyo za wale waliopitiliza katika kuonyesha mapambo – ikiwa ni sahihi kusema hivyo – huenda wakaongoka?

Jibu: Ni wajibu juu ya wanaume kusitiri sehemu za siri. Ikiwa uchi umefunikwa kwa shuka ya chini, kimefunikwa kilicho baina ya kitovu na goti, basi kilichobaki hakidhuru. Lakini ikiwa mavazi yote ni mazuri juu ya mwili, basi hilo ni kamilifu zaidi na zuri zaidi. Lakini muhimu ni kwamba kilicho baina ya kitovu na goti kisitiriwe kwa suruwali au shuka ya chini nzito zenye kufunika, ambazo hazionyeshi fomu ya mwili, si weusi wake wala weupe wake, wala umbo lake. Hili ndilo wajibu. Hali ya wanawake kali zaidi katika hilo kuliko wanaume. Ama baina ya wanaume, basi wanapaswa kufunika sehemu ya miili wao wote, na baina ya wanawake wanafunika sehemu zisizotakiwa kuonekana.

Kwa kumalizia ni kwamba vazi jepesi ni kama aliye uchi. Hii ndiyo maana ya “waliovaa lakini wako uchi”. Kwa  maana ni vazi jembamba au fupi. Huyu yuko mtupu. Vivyo hivyo mwanaume ikiwa ana suruwali ya kupenya au kikoi cha kupenya kinachoonyesha uchi wake, basi hakufunika uchi wake. Tunamuomba Allaah atupe usalama.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3487/نصيحة-لمن-يتهاون-في-ستر-عورته
  • Imechapishwa: 29/08/2026